Home Habari PRISONS YAJIFICHA ZANZIBAR

PRISONS YAJIFICHA ZANZIBAR

5505
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE


TIMU ya Tanzania Prisons imewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

Maafande hao, ambao walimaliza ligi katika nafasi ya nne msimu uliopita, wamepania kufanya makubwa msimu ujao, wakitamba kumaliza moja ya nafasi za juu.

Kabla ya kwenda Zanzibar, timu hiyo iliweka kambi ya siku kadhaa Mpanda, mkoani Sumbawanga.

Wajelajela hao wanajua kuwa wataianza Ligi na mabingwa watetezi, Simba, ambao leo wanatarajiwa kuachana na kambi yao waliyoiweka nchini Uturuki, ndiyo maana wameamua kujipanga mapema.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohamed, alisema nia ya kwenda Zanzibar ni kutokana na utulivu wa kambi, pia kupata mechi nyingi za kirafiki kwa ajili ya kukipima kikosi chake.

“Tunatarajia kukaa huku kwa takribani siku 17 na tukiwa huku tutacheza mechi kadhaa za kirafiki, japo mpaka sasa sijajua ni timu gani tutakutana nazo lakini najua tutapata,” alisema Mohamed.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here