Home Habari Prisons yatema wachezaji saba

Prisons yatema wachezaji saba

920
0
SHARE

prisonsNA MARTIN MAZUGWA

KATIKA kuhakikisha inajiandaa vizuri na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maafande wa Tanzania Prisons wameamua kutema vyota wao saba ili kuanza kujenga timu upya.

Akizungumza na DIMBA, msemaji wa klabu hiyo, Enock Mwanguku, alisema wameamua kuanza kukipangua kikosi chao ili kufanya usajili wa wachezaji wapya.

“Tumewaacha wachezaji saba mara baada ya kupokea ripoti ya mwalimu na hivi sasa tupo kwenye mchakato wa kuziba nafasi za wachezaji hao,” alisema.

Wachezaji walioachwa ni Juma Seif ‘Kijiko’, Ally Manzi ambao wamemaliza mikataba yao, Mohamed Yusuph, Zamkufor Elias. Wengine ni Fredy Edward ‘Chudu’, Adam Chiponga, Bonifasi na Hamis Maingo.

Mwanguku alisema hivi sasa uongozi unafanya jitihada kuongeza wachezaji wenye damu changa ambao wataongeza chachu katika kikosi chake na kuleta ushindani katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here