SHARE

NA BRIGHITER MASAKI

STAA wa muziki wa kizazi kipya nchini Bongo fleva Mwanahawa Abdul, Qeen Darlin pamoja na mume wake Isiaka wamefungua biashara ya kuuza vifaa vya magari na pikipiki kama njia mojawapo ya kutoa ajira kwa vijana.

Akizungumza na DIMBA, Qeen Darlin alisema, kufunguliwa duka hilo kumetimiza ndoto walizokuwa nazo tangu wakiwa wachumba na mara baada ya kufunga ndoa sasa wametimiza lengo lao.

ìTulishapanga tangu tukiwa wachumba hadi sasa tumeoana nia yetu ni kuwasaidia vijana wenzetu kupata ajira na kujivunia sisi kupitia mafanikio yao na huu ni mwanzo tuwakaribishe katika duka letu lilipo Sinza Palestina kwa mahitaji ya vifaa mbalimbali vya pikipiki na magariîalisema Qeen Darlin.

Alisema,mbali na mradi huo pia wanafikiria kitu kingine cha kufanya ambacho kitawaingiziaa kipato lakini pia kutanua soko la ajira kwa vijana wenzao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here