SHARE

CAIRO, Misri

BAADA ya kuhojiwa kwa saa kadhaa, Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, ameachiwa, ingawa uchunguzi dhidi yake unaendelea na atatakiwa kubaki Ufaransa.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa jijini Marseille, Xavier Tarabeux, kigogo huyo wa soka alishikiliwa na mamlaka za Ufaransa kwa tuhuma za rushwa, kuvunja uaminifu na kughushi taarifa.

Itakumbukwa kuwa taarifa ya kukamatwa kwake iliibuliwa juzi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

FIFA walikiri kutambua uchunguzi unaofanywa na mamlaka za Ufaransa dhidi ya Ahmad, wakiongeza kuwa hawana tamko hadi pale kila kitu kitakapokuwa sawa.

“Fifa inaziomba mamlaka za Ufaransa kukabidbhi kila taarifa inayohusika na uchunguzi…” ilisomeka taarifa ya taasisi hiyo kongwe yenye makao makuu yake nchini Uswis.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here