Home Michezo Afrika RAIS WA CAF ATETA NA RAIS WA TUNISIA

RAIS WA CAF ATETA NA RAIS WA TUNISIA

570
0
SHARE
RAIS wa Tunisia, Beji Caid Essebsi

TUNIS, Tunisia

RAIS wa Tunisia, Beji Caid Essebsi, amekutana na ujumbe wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ukiongozwa na Rais wake, Ahmad, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ukaribu wake na Serikali za Afrika.

Taarifa za kutoka Ikulu ya Tunisia zilisema kwamba sababu za kukutana na uongozi wa CAF ilikuwa ni kuimarisha mahusiano baina ya CAF na taifa la Tunisia.

Katika ujumbe huo, Ahmad alisema kwamba nia ya kukutana na kiongozi huyo wa Tunisia, ilikuwa ni kuhakikisha kwamba Serikali hiyo inaendelea kuunga mkono juhudi za kuendeleza soka la Afrika zinazofanywa na CAF, huku Tunisia akiwa ni mdau mkubwa.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri ambayo yameweza kuleta mafanikio kwenye soka la Afrika, tunaamini kwamba ili kufanikiwa ni lazima uwepo uungwaji mkono wa Serikali kwa kiwango kikubwa, huku wakiamini kwamba Tunisia ni moja ya mdau muhimu katika maendeleo ya soka la Afrika,” alisema rais huyo.

Wakati huo huo, Waziri wa Youth na michezo wa Tunisia, Majdouline Cherni, alisema Rais wa Shirikisho la Soka la Tunisia, Wadie Jarie, alikuwa ameweza kufanya kazi kubwa kufanikisha kikao hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here