SHARE

LOS ANGELES, Marekani

JINA la Nipsey Hussle, rapa aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana, limeingia katika kinyang’anyiro cha tuzo za mwaka huu za BET.

Hussle aliyepoteza maisha Machi 31, mwaka huu, ametajwa katika kipengele cha Rapa Bora wa Kiume, akiiwania tuzo dhidi ya wakali J. Cole, Travis Scott, Meek Mill, 21 Savage na Drake.

Kwa upande mwingine, rapa wa kike, Cardi B, amefunika kwa kutajwa katika vipengele saba, kikiwamo kile cha Rapa Bora wa Kike dhidi ya mpinzani wake mkubwa katika muziki wa hip hop, Nicki Minaj.

Aidha, shangwe ni kwa soko la muziki nchini Nigeria, ambapo wasanii wake, Teni, Burna Boy na Mr Eazi, wameingia katika vipengele tofauti.

Hafla ya utoaji tuzo hizo itafanyika Juni 23 katika Ukumbi wa Microsoft Theater jijini Los Angeles.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here