Home Michezo Kimataifa Rashford apigwa mkwara

Rashford apigwa mkwara

566
0
SHARE
Marcus Rashford

LONDON, England

BIG Boss Sam Allardyce amempasha Marcus Rashford kuwa asitegemee kupata namba kwenye kikosi cha England kama ataendelea kusugua benchi Manchester United.

Rashford (18), ni miongoni mwa makinda waliofanya vyema kwenye kikosi cha United msimu uliopita, lakini amejikuta akikosa namba chini ya Jose Mourinho.

Hali hii imemfanya Kocha wa England kukiri kuwa itakuwa ngumu kwake kumjumuisha kinda huyo kwenye kikosi cha taifa, kwa kuwa atakuwa hana uhakika na kiwango chake.

Allardyce alisema: “Kama Rashford atakosa namba kwenye kikosi cha kwanza kwenye klabu yake, itakuwa ngumu kwangu kumuita. Lakini najua uwezo wake ulivyo.

“Katika umri wake, naweza kusema, rudi kacheze kikosi cha vijana U-21, kapate uzoefu kwa kucheza kila siku. Lakini kwa uwezo wake alifika kwenye kikosi cha kwanza msimu uliopita akiwa Man United, ni jukumu lake kupambana ili acheze timu ya taifa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here