SHARE

MADRID, HISPANIA

MARA baada ya kushindwa kupata saini ya kiungo Paul Pogba, klabu ya Real Madrid imemgeukia tena staa wa timu ya taifa ya Brazil na Paris Saint German, Neymar dos Santos, ambaye pia anatakiwa na Barcelona.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, ameamua kumuweka kando Pogba ambaye ndiye alikuwa chaguo lao la kwanza baada ya kiungo huyo kuweka wazi anataka kuondoka Old Trafford, lakini kikwazo kikawa dau lake la Pauni milioni 150.

Neymar, pia ameonyesha wazi kutaka kuondoka katika kikosi cha PSG mara baada ya kuwa na msimu mgumu wa 2018/19 chini ya kocha Thomas Tuchel.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca, rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, hivi sasa akili yake ipo kwa staa wa kibrazili, Neymar baada ya wiki kadhaa zilizopita United kuweka wazi hawapo tayari kumuachia Pogba.

Ripoti kadhaa zimesema wakali hao wa La Liga wapo katika mpango wa kumtoa Gareth Bale pamoja na fedha ili kumng’oa nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here