Home Habari ROONEY AAHIDI MAAJABU BONGO

ROONEY AAHIDI MAAJABU BONGO

419
0
SHARE

NA ALLY KAMWE


MFUNGAJI bora wa muda wote wa Manchester United na Timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney ‘Wazza’, anatua Bongo jioni ya leo na kikosi cha Everton.

Lakini hilo linaweza lisikushtue sana, sikia hii sasa. Kesho Everton watapambana na Gor Mahia ya Kenya, kwenye nyasi za Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, huku Rooney akiahidi kufanya maajabu kwenye mchezo huo.
Rooney alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Everton, akitokea Man United, wikiendi iliyopita, alisema kuwa atautumia mchezo huo kufahamiana na wachezaji wenzake.


“Safari ya Tanzania itanipa nafasi nzuri ya kufahamiana vyema na wachezaji wenzangu pamoja na kujifunza kuhusu mbinu za kocha Ronald Koeman,” alisema Rooney, anayekumbukwa na mashabiki wa soka Bongo kwa bao kali la ‘bicycle kick’, alilowafunga Manchester City, Februari 12, 2011.
Kwa upande wa Koeman, alisema amepanga kumpa kila mchezaji dakika 45 za kucheza kwenye pambano hilo, ili kuwaweka sawa kimwili na maandalizi yao ya msimu.
“Jambo la muhimu kwetu ni kuona tumeanza maandalizi yetu ya msimu kwa kulinda afya za wachezaji wetu. Huu ni mchezo wetu wa kwanza na kila mmoja atacheza kwa dakika 45 tu, alisema Koeman.
Lakini pia raia huyo wa Uholanzi aliongeza kwa kusema kuwa, mara zote huingiza timu uwanjani kwa ajili ya kupata matokeo ya ushindi, hivyo hatakuwa na mzaha wowote kwa Gor Mahia, siku ya kesho.
“Siku zote tunacheza kwa kutaka kushinda na bila shaka tutafanya hivyo pia Tanzania,” aliongeza Koeman na kukiri kuwa, hii ni mara yake ya kwanza kuikanyaga ardhi hii tukufu yenye makinikia ndani yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here