SHARE

NA OSCAR ASSENGA

TIMU ya Mbeya City imeanza kufufua matumaini ya kujinusuru na janga la kushuka daraja baada ya jana kuibamiza bila huruma Lipuli mabao 2-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine.

Mbali na mchezo huo pia Wagosi wa Kaya walishindwa kutumia vyema uwanja wao wa Mkwakwani Tanga, baada ya kupapaswa na Ruvu Shooting mabao 2-1 huku JKT Tanzania wakilazimishwa sare ya 0-0 mbele ya Biashara ya Mara.

Mchezo mwingine ulikua kwenye dimba la CCM Kirumba wakati Mbao wakitumia vyema uwanja huo kwa kuitandika Singida United mabao 3-1 huku Namungo nao wakitakata kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya KMC.

Ushindi wa Mbao unakuja muda mchache baada ya uongozi wa timu hiyo kumtimua kocha mkuu Hemed Morocco pamoja na msaidizi wake Abdulmatik Hajji kutokana na matokeo mabaya mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here