Home Michezo Kimataifa SABABU YA MAJERUHI YA ZLATAN, ROJO YATAJWA

SABABU YA MAJERUHI YA ZLATAN, ROJO YATAJWA

340
0
SHARE

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester United itawakosa nyota wake wawili, Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovic wote kwa msimu mzima uliobakia, baada ya kupata maumivu ya goti kwenye mchezo wa Ligi ya Europa dhidi ya Anderlecht uliopigwa juzi Alhamisi.

Rojo ambaye ni beki tegemeo wa kikosi hicho cha Jose Mourinho, alitegemewa kuonesha dalili za kutokaa nje kwa muda mrefu lakini matokeo ya kiuchuguzi wa kitaalamu yalionesha kuwa jeraha la goti lake la kushoto ni kubwa kuliko ilivyofikiriwa.

Muargentina huyo sasa anasubiri kufanyiwa upasuaji, na huenda asionekane dimbani hadi Septemba mwakani.

Hata hivyo, maumivu aliyokumbwa nayo Ibrahimovic kwenye goti lake la kulia yamegundulika kuwa ni makubwa zaidi ya Rojo, na mfungaji huyo bora wa United msimu huu huenda akakaa nje hadi 2018.

Si jambo la kawaida kwa klabu ya soka kushuhudia wachezaji wake wawili wakipata maumivu yanayofanana kwenye goti ndani ya mechi moja, na jopo zima la benchi la ufundi ndani ya United linaamini majeruhi hayo yanasababishwa na ratiba ya mechi mfululizo zilizofuatana ndani ya wiki za hivi karibuni.

United hadi sasa ndio klabu pekee ya Ligi Kuu England iliyocheza mechi nyingi, ambapo ndani ya mwezi huu ina mechi tisa!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here