SHARE

said

NA JESSCA NANGAWE
SAFARI ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda kufanya majaribio nchini Sweden imeiva, baada ya wakala wake kuthibitisha hati yake ya kusafiria itakuwa tayari keshokutwa.
Ndemla anaweza kuondoka wakati wowote kuelekea katika klabu ya AFC ya Sweden, baada ya visa yake kukamilika.
Akizungumza na DIMBA, Wakala wake, Jamal Kisongo, aliliambia Gazeti hili kuwa, visa yake ilichelewa kidogo kutokana na taratibu za ubalozi, lakini amehakikishiwa kuwa Jumanne itakuwa tayari, hivyo kumruhusu mchezaji huyo kuondoka.
“Visa yake imechelewa kutokana na utaratibu wa ubalozi, lakini tunashukuru klabu yake hiyo imesaidia kuharakisha kutoka kwa hati yake na mpaka kufikia Jumanne kila kitu kitakuwa tayari na Ndemla ataweza kuondoka,” alisema Kisongo.
Mwishoni mwa msimu wa mwaka jana, Simba waligoma Ndemla kwenda kufanya majaribio AFC ya Sweden, ambayo anaichezea Thomas Ulimwengu, kwa kuwa walikuwa wakimhitaji katika mechi zake na sasa wamempa baraka zote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here