SHARE

BIRMINGHAM, England

LICHA ya timu yao kutandikwa mabao 4-0 na Leicester City juzi, baadhi ya mashabiki wa Aston Villa wamemsifia mshambuliaji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta, wakisema hastahili lawama kwa kichapo hicho.

Kupitia akaunti zao za mtandao wa kijamii wa twitter, wengi walisema Samatta alicheza vizuri, japo hakuwa akifikiwa na mipira mingi katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Akitumia jina la Imogen (@imogenxo), mmoja kati ya mashabiki hao wa Villa aliandika: “Nafikiri Samatta ni mchezaji mzuri, tatizo ni kwamba timu haiko vizuri.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mitch (@_g0dmode) aliandika: (Marvelous) Nakamba na Samatta ni watu wawili pekee unaoweza kuwatoa kwenye lawama za kiwango kile kibovu. Kwa ufupi, Villa haina ubora wa kushindana.”

Katika posti nyingine, shabiki aitwaye oliver (@_oliveravfc), aliandika: “Nakamba na Samatta ni wachezaji pekee wa kutolaumiwa usiku wa leo (juzi).”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here