Home Habari SAMATTA AMPA TANO ULIMWENGU

SAMATTA AMPA TANO ULIMWENGU

0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

STRAIKA wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, amepokewa rasmi katika klabu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Sweden, AFC Eskilstuna juzi na tayari amejifunga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Straika mwenzake aliyewahi kukipiga naye katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji, amempa tano Ulimwengu kwa kupata mafanikio hayo.

Samatta alimtumia ujumbe ‘Pacha’ wake huyo aliyecheza naye kwa mafanikio Mazembe akimweleza kufurahishwa na hatua aliyoifikia ambayo yeye alimtabiria siku chache kabla ya kuachana naye.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), alijiunga na Genk Januari 2016 akitokea TP Mazembe ya DRC, walikokuwa wakicheza pamoja na Ulimwengu kabla ya kupata ulaji Genk kumwacha Ulimwengu.

Akizungumza kwa njia ya mtandao, Samatta alisema alipata wakati mgumu kuachana na pacha wake huyo wa uwanjani na aliyaona maisha yangekuwa tofauti sana, lakini alilazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kutafuta maisha.

“Nitakumiss rafiki yangu, lakini haina jinsi ila naamini nitakuwa na wewe si muda mrefu sana, ishi salama,” alisema Samatta akikumbuka moja ya ujumbe aliomtumia Ulimwengu alipokuwa akimuaga.

Kwa upande wake Ulimwengu amewashukuru wote waliochangia kufika hatua hiyo akiwemo wakala wake, Jamal Kisongo na kuahidi kutowaangusha katika safari yake hiyo iliyomfikisha kucheza Ligi Kuu Ulaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here