SHARE

NA SAADA SALIM,

STRAIKA wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, ameshaingia katika rada za kutakiwa na klabu ya Sunderland ya England.

Sunderland, ambao wamewekeza nchini Tanzania kwa kufungua kituo cha kuendeleza soka la vijana (Jakaya Youth Park), kilichopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam, wamekuwa wakiwafuatilia wachezaji wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Klabu hiyo, ambayo ina uhusiano mzuri na Tanzania kwa kutangaza utalii wa nchi hii nchini England, wamekuwa wakivaa jezi zilizoandikwa (Visit Tanzania) pindi wanapofanya mazoezi.

Taarifa za uhakika zilizolifikia DIMBA Jumatano zinadai kwamba, mwishoni mwa wiki klabu hiyo ilimtuma Ofisa wao kwenda nchini Ubelgiji kumfuatilia Samatta katika mechi anazocheza.

Mtoa taarifa huyo alisema Ofisa huyo alikuwapo nchini humo Jumapili wakati Samatta akifunga bao kuinusuru timu yake ya KRC Genk na kipigo kutoka kwa Standard Liege katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji, uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2, kwenye uwanja wao wa nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here