Home Michezo Kimataifa SAMATTA ATAMANI KUTUA KWA MOURINHO

SAMATTA ATAMANI KUTUA KWA MOURINHO

237
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

MARA baada ya kuifungia timu yake ya Genk mabao mawili katika ushindi wa 5-2 dhidi ya mahasimu wao Gent, Mtanzania Mbwana Samatta amesema sasa anatamani kukutana na Manchester United, inayofundishwa na Jose Mourinho hatua inayofuata.

Samatta alifunga mabao hayo mawili katika ushindi huo wakiwa uwanja wa ugenini, mchezo wa Ligi ya Europa na sasa wanasubiri mchezo wa marudiano nyumbani ambapo wakifanikiwa kupata matokeo mazuri watatinga hatua ya nane bora.

DIMBA lilipomuuliza Mtanzania huyo kama timu yake ikitinga hatua hiyo ya nane bora anatamani akutane na timu gani, bila kumung’unya maneno alisema anaitamani Manchester United iliyopo chini ya Mourinho.

“Kwanza niseme nashukuru sana kwa kufunga mabao hayo mawili na kuisaidia timu yangu kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 5-2, kilichobakia ni kupambana mchezo wa marudiano ili tuweze kusonga mbele hatua inayofuata.

“Kuhusu timu ambayo ningependa tukutane nayo hatua inayofuata, binafsi naitaka Manchester United, kwani siku zote ndoto zangu ni kuukanyaga Uwanja wa Old Trafford, nadhani hii itakuwa fursa kubwa kwangu,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here