Home Habari Samatta azidi kung’ara Genk

Samatta azidi kung’ara Genk

1177
0
SHARE
Mbwana Samatta

NA MAREGES NYAMAKA,

KADIRI siku zinavyosogea nyota wa kimataifa Mtanzania, Mbwana Samatta, anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, ndivyo anavyozidi kupanda chati.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, amekuwa msaada mkubwa klabuni hapo baada ya kuwa miongoni mwa nyota walioiwezesha KRC Genk kufuzu hatua ya makundi michuano ya Ligi ya Europa.

Kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi hicho, Mtanzania huyo ameanza kutumika kwenye matangazo ya klabu yake hiyo, ikiwemo michezo yao inayokuwa kwenye ratiba inayofuata.

Samatta, ambaye amesajiliwa na kikosi hicho akitokea TP Mazembe ya Congo, ni moja ya wachezaji wa kutumainiwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheka na nyavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here