Home Habari Samatta: Chad wamenikwaza sana aisee

Samatta: Chad wamenikwaza sana aisee

545
0
SHARE

SamataNA ZAINAB IDDY
NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, amesema kitendo cha timu ya taifa ya Chad kujiondoa katika mashindano ya kuwania kucheza fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Gabon, kimemkwaza kwani kimevuruga mipango yake ndani ya Stars.
Samatta ameliambia DIMBA Jumatano kuwa Stars walikuwa wamejiandaa vya kutosha kupata ushindi mnono katika mchezo huo, hasa baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini, ambapo kitendo cha kujitoa kwao ni kama kimewarudisha nyuma hatua moja.
“Iwapo kama tungeweza kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Chad tungekuwa tumefanikiwa kuwa na pointi saba, ambazo zingetuweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele na hilo lilikuwa linawezekana baada ya ushindi wa mechi yetu  ya awali ugenini,” alisema.
Akizungumzia kufutwa na matokeo yao dhidi ya Chad ambayo yaliambatana na bao lake alilolifunga, alisema wala bao hilo halimuumizi sana na badala yake pointi walizozipoteza ndizo ambazo zinamlaza macho.
“Ni kweli hilo lilikuwa bao langu la kwanza tangu nikabidhiwe kitambaa cha unahodha, lakini haliniumi sana kama tulivyopoteza hizo pointi ambazo zingetufanya kukaa kwenye mstari mzuri,” alisema.
Hivi karibuni Chama cha Soka nchini Chad (FTFA) kilituma barua kwa CAF na TFF kuelezea kushindwa kwao kusafiri kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano dhidi ya Taifa Stars kwa madai ya ukata unaowakabili.
Mchezo huo wa marudiano ulikuwa ufanyike Jumatatu iliyopita, ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wameshakata tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo na iliwalazimu TFF kuwarudishia viingilio vyao jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here