SHARE

MANCHESTER, ENGLAND

KLABU hasimu kutoka jiji moja Manchester United na Manchester City, zimeingia vitani kuwania saini ya kinda wa kimataifa wa England, Jadon Sancho anayekipiga katika kikosi cha Borussia Dortmund ambaye ameonyesha wazi kuwa anataka kuondoka kwa miamba hiyo ya nchini Ujerumani.

Dortmund tayari wameanza kusaka mbadala wa nyota huyo wa kimataifa wa England mara baada ya kukubali kumuachia akatafute changamoto mahala pengine.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, klabu yoyote inayotaka saini ya kinda huyo inapaswa kutoa dau nono huku thamani yake ikiwa pauni milioni 100.

City wanamuangalia kwa ukaribu zaidi kinda huyo ambaye ambaye alikulia katika kikosi hicho kabla ya kumuuza kwa dau la pauni milioni 7 mwaka 2017.

Klabu hizo zinatarajia kuonyeshana umwamba ili kumnasa kinara huyo wa pasi za mwisho nchini Ujerumani ambaye alimaliza akiwa ametoa jumla ya pasi 14.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here