Home Habari SAPRAIZ YA NIYONZIMA YAVUJA

SAPRAIZ YA NIYONZIMA YAVUJA

413
0
SHARE

NA SAADA SALIM

SIMBA wanaendelea kufanya siri juu ya kumtambulisha kiungo wao mpya Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, lakini DIMBA Jumatano limedokezwa kila kitu.
Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa, Niyonzima ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo, baada ya kushindwana na timu yake ya zamani, Yanga na sasa kilichobakia ni kutambulishwa tu.
Mchezaji mmoja wa Simba ambaye alikuwapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, kilichowavaa Rwanda mchezo wa CHAN, alisema walizungumza mengi na Niyonzima na alikiri kumalizana na Simba.
Mchezaji huyo alisema Niyonzima aliwaambia anasubiri kutambulishwa siku ya Simba Day, ndiyo maana mpaka sasa amepiga pozi kwao Rwanda.
“Jamaa (Niyonzima) tulizungumza naye mengi sana na alituhakikishia kuwa ni kweli amesajiliwa na Simba na kwamba atatambulishwa kwenye tamasha la Simba Day, Agosti 8, mwaka huu,” alisema mchezaji huyo.
Kigogo mmoja wa Simba aliliambia DIMBA Jumatano kuwa, wanataka kumtambulisha siku hiyo ya Simba Day, ili kuwachoma moyo wapinzani wao ya jadi, Yanga.
“Tunataka kuwachoma moyo Yanga, ambao baadhi ya mashabiki wao walichoma jezi yake baada ya kusikia kuwa tunamsajili, mashabiki wetu wajiandae kumpokea siku ya Simba Day,” alisema kigogo huyo.
Habari zaidi zinasema kuwa, nia ya vigogo wa Simba kumtambulisha siku ya Simba Day ni kutaka kuuza jezi nyingi za nyota huyo wa kimataifa pamoja na mwenzake Mganda, Emmanuel Okwi.
Inadaiwa kuwa, tayari ‘mzigo’ wa makontena ya jezi za wawili hao umeshawasili na unasubiri kuuzwa siku ya Simba Day.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here