SHARE

LONDON, England

SIKU yoyote kuanzia kesho, usishangae kusikia Juventus wakimtangaza Maurizio Sarri kuwa ndiye bosi mpya wa benchi lao la ufundi.

Taarifa hiyo inaongozana na ile ya staa wa Kibelgiji, Eden Hazard, kukamilisha dili lake la kwenda Real Madrid.

Imeelezwa kuwa tayari pande zote zimeshafikia makubaliano na Juve wamefanikiwa kumrejesha nyumbani Muitalia huyo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Wakala wa Sarri, Fali Ramadani, alikutana na Chelsea juzi na kumalizana nao, hivyo kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 hatakuwa Stamford Bridge msimu ujao.

Sarri alitua Chelsea majira ya kiangazi ya mwaka jana, akichukua kibarua cha Muitalia mwenzake, Antonio Conte, ambaye naye amerudi nyumbani na msimu ujao atakuwa na Inter Milan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here