Home Michezo Kimataifa SASA TUSUBIRI ‘SHOMBO’ ZA WAKALA WA TOURE

SASA TUSUBIRI ‘SHOMBO’ ZA WAKALA WA TOURE

496
0
SHARE

YAYA Toure alipewa dakika 90 za kuthibitisha ubora wake, naye hakufanya makosa, akathibitisha kwa kuimaliza Crystal Palace kwa miguu yake.

Kuna swali jingine Pep Guardiola? Yule ndio Yaya Toure, injini uliyoanza kuichakaza kwa vumbi jukwaani.

Toure amethibitisha ubora wake na ameonyesha bado Manchester City inaweza kumtegemea, sote tulikuwa tunafahamu hili, kasoro mwanadamu mmoja tu ambaye ni Pep Guardiola.

Pep hamwamini Toure, kwanini? Sababu ziko ndani ya nafsi yake.

Alifika City na kumuondoka kikosini kwa sababu dhaifu sana. Mzito, hana kasi na hayuko fiti kimchezo, kwa bahati nzuri haya yote Yaya ameyajibu kwa dakika 90 tu pale Selhurst Park, Toure ametuonyesha ni namna gani anaweza kuwa mchezaji bora wakati wowote anapohitaji.

Mpaka sasa tumeshasikia Yaya akiongea baada ya mechi ya Crystal Palace, tumemsikia pia Pep akionyesha kukosea kwa kutomwamini Yaya, lakini bado mtu mmoja hajazungumza.

Unamjua ni nani? Wakala wa Yaya Toure, Dimitri Seluk.

Nani hataki kuisikia kauli ya Seluk wakati huu? Baada ya kutoleana maneno ya shombo na Guardiola, nani hapendi kusikia neno la kwanza la Dimitri baada ya mabao mawili ya Yaya?

Mwanzoni mwa msimu, Seluk alimshutumu hadharani Guardiola kwa kumpiga benchi Yaya bila sababu, lakini baadaye Yaya akaibuka na kumwomba radhi Pep akiomba nafasi ya kucheza.

Je, si kwamba aliomba nafasi moja ya kucheza ili kutengeneza dili lake la uhamisho kwenye dirisha dogo la Januari mwakani?

Huenda Pep alifanya uamuzi wa busara wa kumpa nafasi Toure lakini pia unaweza kuwa uamuzi atakaokuja kuujutia siku Seluk akifungua kinywa chake.

Mabao mawili ya Yaya yametosha kumsafishia njia yake kwenye usajili, wakati huu Seluk anaweza kuinua simu yake na kuzungumza na klabu yoyote ile, hofu itoke wapi na tayari mteja wake ameshafanya kazi?

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here