Home Michezo Afrika SENEGAL YAREJEA KOMBE LA DUNIA

SENEGAL YAREJEA KOMBE LA DUNIA

743
0
SHARE

POLOKWANE, Afrika Kusini

SENEGAL imefanikiwa kupata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2017, baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0 kwenye mechi ya kufuzu fainali hizo ambayo ilikuwa ni marudio baada ya ile ya kwanza matokeo yake kufutwa.

Senegal maarufu kama Simba wa Teranga, inarejea kwenye fainali za Kombe la Dunia baada kuingia mara ya mwisho mwaka 2002, fainali zilizofanyika kwa ushirikiano wa Korea Kusini na Japan.

Mabao ya Senegal yaliyoifanya kuongoza kwenye Kundi D, yalifungwa na Diafra Sakho likiwa ni bao la kwanza kwenye mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane, kisha Thamsanqa Mkhize alijifunga katika harakati za kuokoa na kufanya mchezo kumalizika kwa wenyeji kutoka vichwa chini.

Kwa matokeo hayo sasa, Senegal inaongoza Kundi D, ikiwa na pointi tano na kutinga rasmi kwenye fainali za Kombe la Dunia ikiwa ni timu tatu kufuzu, timu za kwanza kufuzu ilikuwa Nigeria kutoka Kundi B na Misri ya kutoka Kundi E.

Kufuzu kwa Senegal kwenye fainali hizo imekuwa ni historia mpya kwa timu hiyo lakini pia kwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Aliou Cisse, ambaye wakati wa fainali za mwaka 2002 alikuwa nahodha wa Senegal ambapo moja ya kumbukumbu kubwa ni kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza kisha kuishia hatua ya robo fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here