SHARE

LONDON, England 

NDOTO ya gwiji wa tenisi, Serena Williams, kutwaa taji la 24 la Grand Slam iliyeyuka baada ya kufungwa na Simona Halep katika mchezo wa fainali Wimbledon Open upande wa wanawake uliyochezwa jana jijini London, England. 

Serena ambaye ametwaa taji la Wimbledon mara saba alikua anasaka taji la 24 la Grand Slam ili kufikia rekodi ya Margaret Court lakini sasa itabidi kusubiri na kujaribu tena bahati baadaye mwaka huu katika michuano ya US Open.

Halep, raia wa Romania, alitumia dakika 56 kuzima ndoto ya Serena kwa seti 2-0 (6-2, 6-2) na kuweka historia ya kutwaa taji lake la kwanza la Wimbledon ikiwa pia ni taji lake la pili la Grand Slam.

“Ilikua mechi yangu nzuri,” alisema Halep mwenye umri wa miaka 27 ambapo taji lake la kwanza lilikua French Open mwaka jana.

Kwa Serena aliye na umri wa miaka 37 hii ilikuwa fainali yake ya tatu kupoteza ndani ya miezi 12 na alimpongeza mpinzani wake kwa kuonyesha mchezo mzuri.

Halep ambaye hakuonyesha hofu tangu mwanzo wa mchezo alimzidi mbinu, ujanja na uwezo Serena, raia wa Marekani, na kushinda taji hilo kiulaini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here