Home Burudani SERENA WILLIAMS AREJEA DIMBANI

SERENA WILLIAMS AREJEA DIMBANI

588
0
SHARE
ABU DHABI, Falme za Kiarabu

MASHABIKI wa mchezo wa tenisi duniani, wanaomshabikia mkali wa mchezo huo kwa upande wa wanawake, walikuwa wakiisubiri kwa hamu kubwa jana Jumamosi, ili waweze kumshuhudia tena mkali wa mchezo huo kwa upande wa wanawake, Serena Williams, ambaye alitarajia kurejea tena dimbani.

Serena alitarajia kurejea dimbani jana kucheza na bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa ‘French Open’, Jelena Ostapenko, kwenye michuano ya dunia inayofanyika Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, maarufu kama Mubadala World Tennis Championship, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na michuano mikubwa ya mwakani.

Awali michuano ya Mubadala, inayofanyika kwa siku mbili, ilikuwa ikiwashirikisha wanaume tu kwa miaka 10 lakini mwaka huu wameamua kuwashirikisha pia wanawake, ambapo Serena amekubali kushiriki kama sehemu ya mazoezi.

Serena mwenye umri wa miaka 36, amerejea kwa mara ya kwanza tangu alipojifungua mtoto wa kike aitwaye Alexis Olympia Ohanian, mwezi Septemba.

Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza kwa kipindi cha takribani mwaka mzima, tangu michuano ya Australian Open mwezi Januari.

Mkurugenzi wa Australian Open, Craig Tilley, amesema William anatarajiwa kutetea taji lake katika mechi ya mwaka 2018 ambayo itaanza Januari 15.

Rafael Nadal, Milos Raonic na Stan Wawrinka, wamejiondoa kutoka Mubadala ambayo imechezwa kati ya Desemba 28 na jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here