SHARE

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI mpya wa klabu ya Yanga, umekutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kuhakikisha maslahi ya timu yanalindwa.

Viongozi hao wa Yanga ni wale waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 5, mwaka huu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dkt. Mshindo Msola.

Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa wizara ya hiyo, iliwaonyesha viongozi hao, wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakyembe.

Msola alichaguliwa na wanachama wa Yanga kuingoza klabu hiyo katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi uliopita kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Mwakyembe ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa Yanga kufanya uchaguzi kutokana na hali iliyokuwepo katika klabu hiyo baada ya viongozi wa juu kujiuzulu, huku timu ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here