SHARE

NA KYALAA SEHEYE

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford, amesema haikuwa riziki kwa aliyekuwa mchumba wake, Emmanuel Elibariki, ‘Ney wa Mitego’ kumuoa, licha ya kudumu naye muda mrefu katika mahusiano.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Shamsa, ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na mfanyabiashara aitwaye Rashid, alisema mahusiano yake na Ney wa Mitego yalikuwa mazuri kiasi cha kunusa harufu ya kufunga ndoa, lakini haikuandikwa na Mungu msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya awe mume wake.

“Kila jambo hupangwa na Mungu, kwangu Ney alikuwa mwanamume mwenye upendo na msikivu, lakini kuna mambo madogo yalitutofautisha na kufanya kushindwa kutimiza ndoto zake za kunioa,” alisema.

Alisema, watu wanamsema vibaya Ney, lakini ukweli ni kwamba jamaa hanywi pombe na havuti bangi ambapo anamtakia mafanikio katika maisha yake ya mahusiano aweze kufunga ndoa na mwenza wake.

“Najivunia kuwa kwenye ndoa na nampenda sana mume wangu na nina uhakika ndiye niliyeandikiwa, ila Ney haikuwa riziki yake kunioa,”alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here