Home Habari SHIJA: NINA ASILIMIA 90 ZA KUSHINDA URAIS TFF

SHIJA: NINA ASILIMIA 90 ZA KUSHINDA URAIS TFF

289
0
SHARE

MAREGES NYAMAKA NA MARTIN MAZUGWA

MGOMBEA wa nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Shija Richard, amebainisha kuwa ana asilimia 90 za kushinda nafasi hiyo kwani sera zake zinambeba akiamini wapiga kura hawatamuangusha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Shija amesema anayo nafasi kubwa kutokana na vipaumbele vyake 11 vingine vikiwa vya muda mrefu na mfupi.

“Mipango ya muda mfupi ni kusimamia Azimio la Bagamoyo, uadilifu na utawala bora, kupeleka rasilimali fedha mikoani, kuhamasisha udhamini, maendeleo ya soka la wanawake kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka,” alisema.

Shija ni mgombea wa nafasi hiyo akiingia kwa mara ya kwanza huku akishindana na wenzake watano akiwamo mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay na Wales Karia, ambaye ni Makamu wa Rais katika uongozi wa Jamal Malinzi. Wengine ni Fredrick Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Imani Madega na Emmanuel Kimbe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here