Home Burudani Shilole ajivunia utabiri wa Stars

Shilole ajivunia utabiri wa Stars

379
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongo Fleva na Mjasiriamali, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, amesema ni miongoni mwa Watanzania wachache waliotabiri ushindi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyopata dhidi ya majirani zao Uganda.

Stars iliweza kuitandika Uganda jumla ya mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa mapema mwishoni mwa juma na kuweza kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Shilole ambaye alikuwa ni miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kuisapoti Stars, alisema anashukuru utabiri wake wa mabao matatu umekwenda kama alivyopanga na kujiona ni miongoni mwa Watanzania wachache waliotabiri ushindi huo.

“Najua sitakuwa peke yangu lakini najua pia tupo wachache tuliotabiri matokeo kama yalivyotokea, nilijua Stars itashinda kwa ushindi huo, wengi walijua itashinda lakini si kwa kishindo hicho, hii ndiyo timu ambayo itatufuta machozi Watanzania, naamini itafika mbali,” alisema Shilole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here