SHARE
Zuwena Mohamed ‘Shilole’

NA KYALAA SEHEYE,

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema hajishughulishi kujifunza lugha ya Kiingereza licha ya vijembe anavyotupiwa na wabaya wake kwamba ni maimuna wa lugha hiyo.

Shilole, ameliambia DIMBA kwamba lugha ya Kiswahili aliyonayo inamtosha na ameridhika na maneno machache ya kuokoteza ya Kiingereza ambayo yamekuwa yakimsaidia kuwasiliana na watu mbalimbali.

Alisema anashangaa watu kila kukicha wamekuwa wakimweka mdomoni kuwa hajui Kiingereza wakati maisha yanamwendea kwa kutumia Kiswahili hicho.

“Sioni sababu ya kujifunza Kiingereza, ilimradi najua Kiswahili na Kinyamwezi vinatosha sana hiyo lugha nawaachia wenyewe, ingekuwa siwezi kupata pesa hadi nijue kuongea lugha hiyo hapo kingenihusu ila kama sio basi hakinihusu kabisa,” alisema Shilole ambaye mashabiki wake wanamwita Shishi baby.

“Nakipenda Kiswahili na ninajivunia, mbona China wao wanaabudu lugha yao, tujitahidi kuongea Kiswahili chetu popote ili kukikuza, si kuiga Uzungu tusionao, kwangu mimi watasubiri sana sina mpango,” alimalizia Shilole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here