SHARE

NA BEATRICE KAIZA

MKALI wa muziki wa Injili nchini, Christina Shusho ametoa somo kwa wadada wanaotaka kuolewa wajiweke mbali na wapenzi wao wa zamani kwa kuwa kuwablock kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na DIMBA, alisema, amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa mabinti ambao wameachana na wapenzi wao wa zamani ambao wanawasumbua kwenye mitandao hiyo.

ìNinapokea malalamiko kutoka kwa mabinti kusumbuliwa na wapenzi wao wa zamani ëmaexí kwenye mitandano ya kijamii kitu ambacho kinawafanya kurudi nyuma na kujikuta wanaingia tena kwenye mahusiano ambayo sio sahihi,íí alisema Christina Shusho.

Alisema, wakiwablock itawasaidia kujijenga upya katika maisha bila kutaka kulipa kisasi na kujipatia mtu ambaye ni sahihi katika maisha ya kupata mume bora kwani Mungu anajibu kwa wakati.

Shusho amekuwa akitoa mafunzo mbalimbali kuhusu kutokukata tamaa kwa mabinti pale Dremers Center Manzese Tip-top.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here