Home Michezo Kimataifa SIKIA MKWARA ALIOKUJA NAO CHICHARITO

SIKIA MKWARA ALIOKUJA NAO CHICHARITO

349
0
SHARE

LONDON, England

BAADA ya kutua West Ham United, straika Javier Hernandez ‘Chicharito’, ameitazama beki ya Manchester United na kuwaambia mabosi wake wapya, ‘tuna pointi zetu pale Old Trafford’.

Chicharito aliwahi kuwika akiwa Man United kabla ya kuuzwa Bayern Luverkursen, mwaka 2015, anatarajiwa kucheza pambano la kwanza la Premier akiwa na jezi ya West Ham kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Manchester United.

“Nafikiri itakuwa poa sana kurejea Old Trafford,” alisema. “Kuanza msimu pale ni jambo kubwa kwangu na kwa wenzangu pia, nina hakika tutapata pointi tatu.

“Nimefarijika mno kurejea katika ligi bora duniani. Ni faida kubwa sana kwangu kama mchezaji. Lengo letu ni kucheza Uropa, hivyo ni lazima tucheze vizuri karibu kila mchezo.

“Slaven Bilic amekuwa mchango mkubwa mimi kuja hapa. Tangu nilipojiunga na Bayer Leverkusen, tumekuwa tukiwasiliana sana. Nimekuja na niko tayari kufanya naye kazi,” alisema Chicharito.

Akiwa Manchester, Chicharito alifunga mabao 59 kwenye michezo 157 aliyocheza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here