Home Michezo Kimataifa Silva: Messi amezoea kuwachezea na waamuzi

Silva: Messi amezoea kuwachezea na waamuzi

0
SHARE

RIO, BRAZIL

NAHODHA wa timu ya taifa ya Brazili, Thiago Silva, amesema kuwa staa wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ni mwepesi kukasirika kwani kitendo alichofanya katika mchezo dhidi ya Chile sio mara ya kwanza aliwahi kufanya hivyo katika mchezo wa klabu bingwa ulaya kati ya Barcelona na Paris Saint-Germain mwaka 2017.

Nyota huyo wa Argentina alisema kuwa michuano hiyo iliyofanyika nchini Brazili imethiriwa na rushwa  kutokana na jinsi inavyoendeshwa.

 “Labda nimelipwa kwa kile nilichosema wakati uliopita,”alisema Messi mara baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu.

Beki huyo wa Brazili alijibu kuwa Messi alipata faida katika mchezo ambao Barca walipopata matokeo ya kushangaza ya ushindi wa mabao 6-1 miaka miwili iliyopita.

“Ni ngumu kujibu katika ujumbe, wakati mwingine tunaposhindwa tunapaswa kuwafikiria na wengine,” alisema Silva mara baada ya Brazil kuibuka na ushindi wa mabao  3-1 dhidi ya Peru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here