Home Habari SIMBA HII UTAIPENDA TU

SIMBA HII UTAIPENDA TU

7135
0
SHARE

EZEKIEL TENDWA NA SAADA SALIM         |     


KWA sasa ukitaja timu zenye mastraika bora katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, huwezi kukwepa kuwataja mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ambayo imesajili karibu kona zote na kutengeneza safu hatari ya ushambuliaji.

Kikosi hicho tayari kimeshaanza kumtumia Meddy Kagere iliyemsajili akitokea Gor Mahia ya Kenya atakayeungana na  Emmanuel Okwi Raia wa Uganda, Kakule Fabrice Raia wa DRC aliyeanza mazoezi na kikosi cha Simba wiki hii, huku mipango ya kumnasa kiungo Francis Kahata ikipamba moto.

USAJILI KAMILI

Katika usajili walioufanya mpaka sasa, Simba imeongeza mastraika wanne kutoka katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambao msimu uliopita waliwasha moto katika timu walizotoka, hiyo ikimaanisha kuwa watakapoungana na John Bocco na Emmanuel Okwi, kikosi kitakuwa na fowadi kali sana hapa nchini.

Simba imemsajili Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya Kenya, ambaye msimu uliopita alimaliza nafasi ya pili Ligi Kuu nchini Kenya akiwa na mabao 14 na msimu huu alifunga mabao nane kabla ya kuondoka.

Kagere ni mmoja wa washambuliaji wa kuogopwa katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hivyo kusajiliwa Simba kunatajwa kuwa kutaleta mchango mkubwa katika maandalizi ya michuano yao ya kimataifa.

Pia wamemsajili Marcel Kaheza kutoka Majimaji ya Songea, ambaye alimaliza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita akiwa na mabao 14 sawa na nahodha wa Simba, John Bocco ambao walishika nafasi ya pili nyuma ya Okwi aliyefunga jumla ya mabao 20.

Baadaye walimsajili Adam Salamba kutoka Lipuli FC, ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao saba katika nafasi ya 11 akilingana na Ibrahim Ajib wa Yanga pamoja na Shiza Kichuya wa Simba.

Jumla ya mabao hayo ya washambuliaji wa Simba, yanatoa picha halisi kwamba timu itakayokaa vibaya msimu ujao, inaweza kupata kipigo cha aibu.

Kutokana na upana wa kikosi hicho cha Simba hasa safu yake ya ushambuliaji, kocha wake mkuu, Masoud Djuma, amewahakikishia Wanasimba kuanza kufaidi matunda ya ushindi katika mechi za ndani na za kimataifa.

MKWANJA MNENE

Mbali na hilo, pia Simba inatajwa kuwa kinara kwa mkwanja kati ya timu zote 16 zilizoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, huku Wekundu hao wa Msimbazi wakitwaa ubingwa.

Katika mapato ya mlangoni, Simba walikusanya Sh 380, 867, 592, ikifuatiwa na wapinzani wao wa jadi Yanga waliokusanya jumla ya Sh 257,113, 365, Lipuli FC wakishika nafasi ya tatu wakikusanya Sh 71, 908, 665, Singida United 68,939, 621 na Mbeya City wakishika nafasi ya tano wakikusanya Sh 54, 766, 008.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, hayo ni mapato ya mlangoni.

Alisema timu zinapata asilimia 40 wakiwa uwanja wa nyumbani na asilimia 20 wakiwa uwanja wa ugenini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here