SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi – mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri naoî.

Huo ni ujumbe wa bilioenea kijana Afrika, Mohamed Dewji ëMOí ambaye ni mwekezaji wa Simba ambayo kwa upepo ulivyo sasa ni wazi kuna mambo yanadhihiridha hayako sawa baina yake na uongozi.

Bahati mbaya usiri umetawala katika hilo.Majibu mengi yanayotoka vinywani mwa baadhi ya viongozi wa juu ni ya kisiasa sana. Hadi siku MO mwenyewe atakapoamua kulieleza kiundani mbele ya vyombo vya habari pale gorofa ya 20 Golden Jubilee Towers.

Kwa haraka haraka tu unajiuliza kama kuna mtu anatoboa jahazi ni kwa nini anafanya hivyo?Kwa maslahi gani? Bila kumuhumu hata kabla ya kujua jina lake huenda ana jambo la msingi sana.
Mfumo wa mpya wa uendeshaji ndo kwanza ndo mwanga unaanza kuoneakana kwa mbali, ghafla tu kuna kiza kinataka kufunika. Maana yake ni nini? Ni sawa na kupiga hatua tano mbele, unarudi nyuma saba.

Miaka nenda, rudi nani hajui kama Simba na Yanga zinafanikiwa kufanya vizuri kwa ukubwa wa pochi ya Mwenyekiti wa wakati huo? Mikakati ya klabu klabu kujiendesha yenyewe ni kama wimbo tu uliozeeleka.

Ugumu wa jambo jipya na vikwazo vya hapa na pale pale havijawahi kukosekana, huenda hiki ndicho kinaonekana ndani ya Simba ambayo chini ya MO imeponya maumivu ya kukaa misimu mitano bila kutwaa ubingwa wala kushiriki michuano ya kimataifa.

Nani anaweza kunyoosha kidole juu kuhoji kilichofanywa na MO ndani ya timu hadi sasa hivi? Hakuna kuanzia usajili wa wachezaji, malazi, mishahara yao na posho pochi ya MO imefunguka kweli kweli.

Nanong’onezwa na mwanachama mmoja kwamba kuna kundi linahitaji ile bilioni 20 iingie kwenye akaunti mambo mengine yaendelee. Ni sawa, lakini ni suala la utaratibu tu. Halafu nyie Wanachama wenye asilimia 51 ya hisa hadi sasa mmeingiza kiasi gani? Hapo pagumu.

Simba ni kubwa kuliko mtu yeyote, Simba inatakiwa iendelee kuwa kioo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuvuka pale ilipofikia msimu uliopita robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari usajili unaonyesha dhamira aliyonayo mwekezaji kushindana na timu za madaraja ya juu, Al Ahly, TP Mazembe, Zamalek, Waydad Cansablanca halafu ghafla tu linatokea suala kutoboa mtumbwi. Ukakasi.

Ukweli mchungu, lakini dawa Simba inamuhitaji MO kuliko yeye anavyohitaji. Hakuna tajiri ambaye haitaji mafanikio, lakini unatengeza kwanza hiyo njia ya mafanikio kwanza kwa utulivu mkubwa.

Kama mtu anatokea anahoji kwamba kiasi cha milioni 250 kwa mwaka kutoka kwa udhamini MO Xtra ambayo ni kinywaji kutoka miongoni mwa Makampuni ya MO ni kiduchu ni tatizo.

Kabla ya hapo Simba ilikuwa na wadhamini wangapi? Hakuna jibu la kuridhisha ni mazoea ya kujadili mambo mepesi kwa jicho la kawaida. Kuna mambo mawili muhimu.

Kwanza ni meza ya majadiliano kati ya upande wa MO pamoja na wajumbe wa bodi ya klabu wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Swedy Nkwabi, kila mmoja akiwa na kabrasha lake la katiba.

Lakini ikiwa bado ni ngumu maamuzi ya mwisho huwa yanatoka kwa wenye timu yao(Wanachama) kupitia mkutano Mkuu kama walivyopitisha kwenda kwenye muundo mpya, ndivyo itakavyokuwa waendelee naye au wamuweke pembeni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here