SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

SIMBA inanoga tu, wala hakuna ubishi hii inatokana na kuendelea kupata matokeo mazuri katika michuano ya Ligi Kuu, huku safu yake ya ushambuliaji ikionekana kuwa moto zaidi.

Mabiwa hao watetezi wamethibitisha hilo jana, baada ya kuishindilia Ruvu Shooting mabao 3-0 na kurejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya juzi kiushushwa na Kagera Sugar.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa Straika kinda machachari Miraji Athuman, akigeuka lulu ndani ya kikosi baada ya kuifungia timu yake mabao mawili kati ya ushindi huo wa 3-0.

Simba ikiwa chini ya kocha wake Mbelgiji Patrick Aussems, ilifanikiwa kutawala mchezo kipindi cha kwanza kabla ya straika Miraj Athuman ëShevaí kupachika bao kwa kichwa akipokea krosi ya Shomari Kapombe katika dakika ya 39.

Hadi timu zote mbili zinakwenda mapumziko ni Simba walioondoka na faida ya bao hilo, lililowapa furaha mashabiki waliofurika katika uwanja huo.

inakwenda mapumziko ni Simba walioondoka na faida ya bao hilo, lililowapa furaha mashabiki waliofurika katika uwanja huo.

Hata hivyo huenda Simba ingetoka kifua mbele kwa idadi ya mabao mengi endapo ingetumia vizuri nafasi walizopata wachezaji wake hasa katika kipindi cha pili.

Wekundu hao wa Msimbazi walifika mara nyingi langoni kwa maafande hao, lakini kosakosa zilitawala zaidi huku wachezaji wengi wakikosa nafasi za wazi.

Mbrazil Gerson Fraga wa Simba itabidi ajilaumu mwenyewe baada ya kushindwa kuweka mpira kimiani akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Francis Kahata, lakini kutokana na kukosa umakini akapaisha mpira huo juu ya lango la Ruvu Shooting.

Fraga alikosa bao tena dakika ya 37 baada ya kupiga kichwa mpira uliochongwa na Pascal Wawa na mpira huo kutoka juu ya lango.

Hata hivyo mchezo huo haukuwa rahisi kwa Simba kwani Ruvu Shooting licha ya kupokea kichapo hicho, lakini walionekana imara hasa eneo la ushambuliaji ambapo mara kadhaa walilitia msukosuko lango la mabingwa watetezi hao lililokuwa likilindwa na kipa wao namba moja, Aishi Manula.

Ushindi huo umeifanya Simba kurejea kileleni ikiwa imecheza mechi 10 na kujikusanyia pointi 25, ikifuatiwa na Kagera Sugar iliyoshushwa kileleni ikiwa na pointi zake 23, ikicheza michezo 11.

Kikosi cha Simba kiliwakilishwa na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Tairone Santos, Pascal Wawa , Gerson Fraga, Hassan Dilunga/Deo Kanda, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere/Ibrahim Ajib, Miraji Athuman na Francis Kahata/Shiboub Ruvu Shooting; Mohamed Makata, Omary Kindamba, Kassim Simbaulalanga, Renatus Ambro, Rajab Zahir, Zuber Dabi, Emmanuel Martin, Shaban Msala/Mosses Shabaan, Sadat Mohamed, Said Dilunga/Fullyzuzu Maganga, na Edward Christopher/Abdulhaman Musa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here