Home Habari Simba mpya kujifua Uturuki

Simba mpya kujifua Uturuki

656
0
SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

SI unakumbuka msimu uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba waliweka kambi nchini Uturuki? Sasa ni kama wamenogewa na inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kikosi hicho kikiwa na nyota wake wapya msimu huu watakwenda kupiga kambi tena nchini humo.

Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems, aliyepo mapumzikoni nyumbani kwao  katika kitongoji cha Moelingen nchini Ubelgiji aliliambia DIMBA Jumatano kwamba alivutiwa kwa kiasi kikubwa na kambi hiyo, baada ya kuona wachezaji wake wamerudi wakiwa fiti na kufanya vizuri katika michezo ya ligi na ya kimataifa.

“Nimechagua kurudi tena Uturuki, ni sehemu nzuri kwa wachezaji kujijenga kisaikolojia pamoja na kuweka miili yao sawa kutokana na hali ya hewa,” alisema Aussems.

“Pia Uturuki ni nchi ambayo ina madaktari wazuri wa viungo, hivyo nahitaji wachezaji wangu wote wakafanyiwe uangalizi wa afya kabla ya kuanza msimu.”

Kocha huyo aliongeza kuwa kambi hiyo safari hii itasaidia kwasababu watacheza mechi za kirafiki na timu ambazo ziliomba msimu ule lakini ikashindikana kutokana na muda.

Mbelgiji huyo bado anaendelea na likizo yake ya mwezi na atarejea kwa ajili ya maandalizi na kuangalia wachezaji wapya ambao wamesajiliwa kulingana na ripoti yake aliyoikabidhi kwa uongozi wa klabu hiyo hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here