Home Habari Simba sasa mwendo wa magari tu

Simba sasa mwendo wa magari tu

1009
0
SHARE

Na Mwandishi Wetu

KWELI Simba msimu huu wamepania!
Huu ndio ukweli uliopo hivi sasa, baada ya wadau wa klabu kongwe ya soka nchini, Simba, kuamua kuwa karibu na timu yao, hasa katika kipindi hiki cha ushiriki wa Ligi Kuu Bara, ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope, ameonyesha jeuri ya fedha kwa kumkabidhi gari beki kisiki, Mohamed Hussein Tshabalala, huku akiahidi kuendelea kutoa zawadi kama hizo kwa wachezaji wengine.

Ahadi hiyo kwa kiasi kikubwa imeamsha ari ya kujituma ndani ya kambi ya klabu hiyo, ambapo Dimba limedokezwa kuwepo na ushindani wa hali ya juu katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika kambi ya Polisi, iliyopo Kilwa Road, jijini Dar.

Wakati Tshabalala akianza maisha mapya kwa kusafiri katika gari aina ya Toyota Raum, Hans Pope amesema wachezaji wengine wanaojituma kikosini, Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wamo katika rada za mwisho kuinasa zawadi kama hiyo.

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, muda mfupi baada ya timu yake kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika Uwanja wa Uhuru Jumapili iliyopita, alisema ari imeongezeka katika kikosi chake kutokana na ugumu wa kupata namba katika kikosi cha kwanza.

Lakini hata hivyo, Dimba linafahamu kwamba licha ya ukweli wa kauli hiyo, kuwepo kwa zawadi za magari na pia zawadi za fedha taslimu zinazotolewa na vigogo wa klabu hiyo kumezidisha ushindani na wachezaji kujituma zaidi.

Tayari wachezaji wa timu hiyo wameshalipwa Sh milioni 20, ikiwa ni zawadi ya ushindi kwa mechi mbili, moja ilipoifunga Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 na kisha kuitandika Mtibwa Sugar kwa jumla ya mabao 2-0.

Mkakati mwingine wa vigogo wa klabu hiyo ni kuhakikisha timu inapata ushindi katika mechi zake tatu zijazo, ikiwemo ya watani wao wa jadi, Yanga, itakayochezwa Oktoba 1.

Mechi nyingine ni kati ya Simba na Azam FC, itakayochezwa Septemba 17 na Wekundu hao wa Msimbazi dhidi ya Majimaji ya Songea inayotarajia kuchezwa Septemba 24.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here