Home Habari SIMBA YA MO, ITAPENDEZA

SIMBA YA MO, ITAPENDEZA

2832
0
SHARE

 

KAMA Simba mpya chini ya mwekezaji wao, Mohamed Dewji ‘Mo’, itafuata masharti mapya yaliyowekwa na ABDUL MKEYENGE

Serikali, bila shaka itapendeza zaidi kuelekea kwenye mafanikio wanayoyataka ndani na nje ya nchi.

Awali ilitajwa kwamba Mo amechukua hisa ya 51%, huku Simba ikibaki na hisa 49%, lakini Serikali ilijitokeza na kusema kwa mujibu wa kanuni, mwekezaji  amechukua hisa 49% na klabu itabaki na hisa 51%.

Akizungumza na DIMBA Jumatano jana, Msajili Mkuu wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa, alisema kanuni 28 A sehemu ya kwanza, inaeleza kuwa klabu iliyoanzishwa na wanachama ikitaka kuuza hisa zake inatakiwa iuze hisa 49% kwa mwekezaji na klabu ibaki na hisa 51%.

Alisema kikao cha Serikali na wadau kilichokaa Oktoba 27, mwaka huu, kilipitisha maazimio hayo ambayo kwa sasa ndiyo kama sheria.

“Sioni kama kuna ugumu hapa. Hizi kanuni ziko kisheria na ziko wazi kabisa kwa klabu zilizoanzishwa na wanachama zikitaka kuuza hisa zake zenyewe zibaki na hisa 51% na mwekezaji awe na hisa 49%.

“Hata Simba wanajua hivi na tuliwatumia hadi nakala. Kama kutakuwa na mabadiliko mengine ya kikanuni au sheria, tunaweza kuketi chini na kutazama upya mchakato huu, lakini kwa sasa tunasimamia hapo kwa 51% klabu na 49% kwa mwekezaji,” alisema Mkwawa.

Mkwawa aliongeza kuwa Simba ilipaswa kuwaambia wanachama wake kuwa hisa 49% zinakuwa za mwekezaji na hisa 51% zinakuwa za wanachama.

Alisema alishangaa kuona mkutano wao wa mwishoni mwa wiki ulimalizika bila viongozi kuwafafanulia wanachama wao juu ya hisa 49% na 51%.

“Sitaki kuwa msemaji wao, lakini Simba walipaswa kuwaweka wazi wanachama wao ili kuondoa hizi sintofahamu zilizotanda huku mitaani.

“Viongozi wanafahamu hiki kitu kwa maana tuliwatumia kabla ya kikao, lakini nikashangaa katika mkutano ule wamekaa kimya, sitaki kuwa msemaji wao, lakini hapa walitakiwa kupazungumza,” alisema.

Mkwawa alieleza kuwa Serikali imeshatunga kanuni kwa ajili ya kuziongoza klabu zote ambazo zinamilikiwa na mwanachama na zikitaka kwenda kwenye mfumo wa uwekezaji kwa njia za hisa, sasa wazisome kanuni zilizotungwa na Serikali kuwa mwanachama anatakiwa kumiliki hisa 51% na mwekezaji hisa 49%.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here