SHARE

NA JESSCA NANGAWE

Ndivyo wanavyojipa moyo viongozi wa Simba na sasa inajiandaa vyema kushinda mechi mbili za kanda ya Ziwa ili kurejesha imani ya mashabiki wao.

Simba ambayo imetoka kwenye jeraha la kupoteza mchezo wa fainali Kombe la Mapinduzi mbele ya Mtibwa Sugar, imeapa kurudisha tabasamu kwa mashabiki kwa kushinda mechi hizo mbili ambazo zitaipa pointi 6 na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi..

Mzuka wa Simba unaongezeka zaidi hasa baada ya tajiri wa klabu hiyo Mohammed Dewji ‘Mo’ kubatilisha kauli yake ya kutaka kujiengua nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi kufuatilia matokeo mabaya waliyoyapata kwa siku za hivi karibuni huku akiwapa moyo wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.

Kikosi hicho kikiwa chini ya kocha wao Sven Vander Broeck ,tayari kimetua jijini Mwanza kwa michezo yake miwili ambapo kesho itajitupa uwanjani dhidi ya Mbao Fc, kabla ya Jumapili kuwavaa Alliance kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Akizungumza na DIMBA Kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola alisema wamesahau matokeo yaliyopita na sasa nguvu zao wanazielekeza katika mechi za ligi zilizo mbele yao ili kutetea ubingwa wao.

Alisema wanakwenda kupambana katika michezo miwili ndani ya Jiji la Mwanza, huku wakiamini michuano ya Mapinduzi imekua sehemu ya mafunzo kwao ya kutekeleza majukumu yaliyo mbele yao kwa sasa.

“Tumepoteza kombe, haina maana tutajibweteka, bado tuna kazi ngumu mbele yetu, wachezaji wanahitaji kupewa moyo na sapoti kubwa ili tutimize kile tulichodhamiria,ligi inatuhitaji na ubingwa tunautaka tena kwa mara nyingine, tunarudi kupambana”alisema Matola.

Aidha Matola alisema huu si wakati wa mashabiki wa Simba kuwanyooshea vidole wachezaji wao bali kikubwa ni kuhakikisha wanazidi kuwapigania na kushirikiana nao ili waweze kutimiza malengo.

Simba ambao ni vinara wa Ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 35 mpaka sasa, wanakabiliwa na michezo miwili Katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here