Home Habari Simba yahusika na ubingwa wa Yanga

Simba yahusika na ubingwa wa Yanga

677
0
SHARE

KIKOSI-1NA EZEKIEL TENDWA

YANGA wapo katika spidi kubwa ya kutaka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini kama hujui Simba nao wanalalamikia Wanajangwani hao kubebwa hadi kufikia hatua hiyo wanahusika kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wapinzani wao hao wa jadi.

Unajua ikoje? Simba ni moja ya timu ambazo zimefungwa ndani nje na Yanga na kama Wekundu hao wa Msimbazi wangejitutumua wakashinda michezo yote miwili wangejikusanyia pointi zote sita na sasa wangekuwa na pointi 64 ambazo bila shaka zingekuwa msaada kwao kusaka ubingwa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ulichezwa Septemba 26 mwaka jana Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Simba walijikuta wakitoka vichwa chini baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0.

Kama hiyo haitoshi Simba walijikuta tena wakipokea kipigo kama hicho mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Februari 2 mwaka huu, hivyo msimu huu Simba wakikubali kufungwa jumla ya mabao 4-0.

Kwa sasa Simba wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 58 baada ya kushuka uwanjani mara 25 wakishinda michezo 18 na kupoteza mine, huku wakitoka sare michezo minne ambapo mchezo ujao watakutana na Mwadui Uwanja wa Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here