Home Habari SIMBA YARUKA MTEGO WA YANGA

SIMBA YARUKA MTEGO WA YANGA

465
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE,

SIMBA bwana wanajifanya wajanja sana, eti wanadai wameshtukia mchezo mchafu ambao unataka kufanywa na mahasimu wao, Yanga, endapo tu watakwenda kizembe katika ziara yao ya Kanda ya Ziwa na hivyo wamebadili mipango fasta.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa, Yanga wametuma mashushushu Kanda ya Ziwa kufanya fitina zote ili kuhakikisha Simba wanashindwa kutimiza ndoto zao za kuchukua ubingwa msimu huu.

Simba wanahitaji pointi 18 ili waweze kutawazwa mabingwa msimu huu, pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Katika pointi hizo, wenyewe wanaamini kwamba, kazi kubwa itakuwa katika michezo yao mitatu itakayopigwa Kanda ya Ziwa ambapo timu hiyo itacheza na Kagera Sugar, Toto Africans na Mbao FC.

Awali Rais wa Simba, Evans Aveva, aliliambia Dimba kuwa wanatarajia kwenda Bukoba mapema kuweka kambi huko kujiandaa na michezo hiyo mitatu.

Hata hivyo, baadaye alibadilisha kauli hiyo na kubainisha kwamba, suala la kambi hata hivyo litategemea kukamilika kwa michakato yao ambayo hakuibainisha, hali ambayo inaonyesha kiongozi huyo kutotaka kuweka wazi mipango yao kwa kuhofia hujuma.

“Tumepanga kwenda Kanda ya Ziwa mapema, ila hatujajua kama tutakuwa Mwanza au Bukoba, tukishamaliza kucheza na Madini FC huku Arusha michuano ya FA ndipo tutajua wapi tunakwenda,” alisema Aveva.

Hata hivyo, aliongeza kuwa endapo ratiba ya Ligi kuu itabadilishwa, wanaweza kurudi Dar es Salaam kwanza na baadaye kwenda Kanda ya Ziwa, japo malengo yao yalikuwa ni kutokurudi Dar es Salaam baada ya mchezo wao wa kirafiki wa jana dhidi ya Polisi Dodoma, uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 55, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 53.

Simba ina hamu ya kupata ubingwa msimu huu baada ya kuukosa kwa miaka minne mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here