Home Habari Simba yawinda saini ya Chilunda

Simba yawinda saini ya Chilunda

757
0
SHARE

NA TIMA SIKILO

STRAIKA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shabaan Chilunda, ambaye amevunja mkataba wake na timu ya soka ya Tennerife ya nchini Hispania inadaiwa anawindwa na klabu ya Simba kwaajili ya msimu ujao.

Azam FC walimtoa Straika huyo kwa mkopo wa miaka miwili ambapo kwa sasa yupo nchini akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Stars wanaojiandaa kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Afrika zitakazofanyika baadaye mwezi huu nchini Misri.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka upande wa Azam FC kililiambia DIMBA kuwa, kwasasa mchezaji huyo anawindwa na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba.

Alisema pamoja na timu hiyo kuhitaji saini ya Chilunda lakini wao pia wanahitaji huduma yake hivyo mchezaji mwenyewe ataamua nini cha kufanya kwa wakati muafaka.

“Chilunda amevunja mkataba wake kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kama ambavyo mwenyewe alikuwa anahitaji ili dunia imuone. Simba wanamuhitaji na Azam FC wenyewe wanamtaka lakini yeye mwenyewe ndio mwamuzi wa mwisho,” alisema.

Chilunda ni miongoni mwa washambuliaji kinda ambao wapo kwenye historia ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here