Home Habari SINGIDA UNITED ‘MCHAWI’ KUAMUA UBINGWA

SINGIDA UNITED ‘MCHAWI’ KUAMUA UBINGWA

7643
0
SHARE

 

NA CLARA ALPHONCE

UWANJA wa Namfua Singida, umeonekana kuwa mgumu kupata matokeo kwa Yanga, hali hiyo imewashtua Simba ambao wanatarajia kwenda kucheza na Singida United katika uwanja huo mchezo wa Ligi Kuu Tanznaia Bara.

Yanga walishindwa kupata matokeo kwenye Uwanja wa Namfua, baada ya kutoka suluhu na Singida United, hivyo juzi kutolewa katika michuano ya Kombe la Azam (FA) kwa penalti 4-2 na wenyeji Singida katika uwanja huo huo.

Mashabiki wengi wa Wekundu wa Msimbazi wameanza kupata wasiwasi kuwa Singida United inaweza kuwa kikwazo kwao kupata matokeo mazuri katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa katika uwanja huo.

Katika mchezo wa awali waliocheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Yanga pia wanatarajia kukutana na Singida kwa mara nyingine katika Uwanja wa Taifa, mchezo wa Ligi Kuu, baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia, mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajia kufanyika Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba na Yanga pamoja na Azam FC, wapo katika harakati za kuwania kutwaa ubingwa msimu huu. Huku kila mmoja akiwa anamuombea mwenzie dua mbaya ili aweze kupoteza mchezo kati ya michezo iliyobaki.

Wakongwe hao wa soka nchini wamefungana kwa pointi, huku kila mmoja akiwa na pointi 46, ila Simba wakiwa mbele kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Simba wanahitaji zaidi ubingwa msimu huu kuliko kitu chochote baada ya kuukosa kwa misimu mitano mfululizo, huku Yanga ikichukua mara tatu mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here