Home Michezo Kimataifa SIRI YA MARTIAL KUTUPIA MABAO HII HAPA

SIRI YA MARTIAL KUTUPIA MABAO HII HAPA

750
0
SHARE

MANCHESTER, England

KOCHA wa klabu ya Man United, Jose Mourinho, amesema kinachomfanya winga wake, Anthony Martial, awe moto msimu huu ni kuwa na furaha tu.

Msimu uliopita Martial alikuwa akipondwa sana na Mourinho kutokana na kiwango cha chini, akifunga mabao nane tu kulinganisha na 17 aliyofunga msimu wake wa kwanza United.

Lakini hadi kufikia sasa, Martial ana mabao manne na Mourinho alisema fomu ya Mfaransa huyo inasababishwa na furaha aliyonayo muda wote.

“Siku hizi ana hamasa, usoni mwake ni mtu mwenye furaha, mwili wake una hamu ya kucheza soka,” alisema Mourinho.

“Ukitaka niseme neno moja, ni furaha tu”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here