SHARE

NA JESSCA NANGAWE

WAKATI kesho Taifa Stars uikirusha karata yake ya pili dhidi ya Kenya kwenye michuano ya AFCON msanii Snura Mushi amesema Stars itaanza safari yake hapo.

Akizungumza jana, Snura ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba alisema pamoja na Stars, kuanza vibaya michuano hiyo dhidi ya Senegal, lakini anaamini tayari wamejirekebisha makosa na safari yao mafanikio itaanza kesho.

“Tulianza vibaya lakini haina maana  tukate tamaa, Wakenya tunawajua, ni timu ya kawaida, nadhani mwalimu ameona makosa katika mchezo wa kwanza na tayari wameyafanyia kazi”Alisema Snura.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Kenya ili iweze kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo inayoendelea nchini Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here