Home Michezo Kimataifa Solskjaer: Hata Europa ‘fresh’ tu

Solskjaer: Hata Europa ‘fresh’ tu

0
SHARE

MANCHESTER, England

KAMA ulidhani inaweza kumsikitisha kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, kushiriki katika michuano ya Ligi ya Europa msimu ujao, utakuwa umekosea.

Solskjaer aliyeichukua timu hiyo Desemba mwaka jana alisema michuano hiyo inaweza kumsaidia kujenga kikosi hicho huku akitaka timu yake waichukulie ‘siriaz’.

Kocha huyo raia wa Norway na mchezaji wa zamani wa Manchester United alidai Ligi ya Europa ikitumika vizuri kwao wataweza kurudi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Si vibaya kushiriki Ligi ya Europa, miaka miwili iliyopita tulishinda taji hili na kurejea michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Najua si rahisi lakini Chelsea na Arsenal walifanya vizuri msimu uliopita katika michuano hiyo ya Ulaya, naamini itatusaidia kujenga kikosi chetu,” alisema Solskjaer.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here