KLABU ya Southampton inajiandaa kumpa mkataba mpya kocha wao, Ronald Koeman, ili abaki klabuni hapo msimu ujao.
‘Saints’ wanataka kumbakisha kocha huyo baada ya ripoti mbalimbali kusema kwamba vigogo kadhaa barani Ulaya vinamtolea macho Mdachi huyo, anayefanya vizuri kwa sasa.