Home Habari SPIDI 120! KWA MAN CITY ILE, MOURINHO ANAFUKUZA UPEPO TU

SPIDI 120! KWA MAN CITY ILE, MOURINHO ANAFUKUZA UPEPO TU

723
0
SHARE

MANCHESTER, England

USHINDANI unaooneshwa na kikosi cha Manchester City kinachoongozwa na  Pep Guardiola katika Ligi Kuu England msimu huu, ni wazi kwamba unatoa changamoto kubwa kwa Jose Mourinho kutimiza lengo la United.

Manchester City ambao wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na tofauti ya pointi nane na United wenye pointi 23, wanampa wakati mgumu Mourinho ambaye kwa sasa anasumbuliwa na presha za mashabiki wa timu hiyo ambao hawapendezwi na kiwango cha timu yao.

Kutokana na hali hiyo, Mourinho anatakiwa kuwa na hofu kuhusu kikosi cha Guardiola kutokana na kiwango chake msimu huu badala ya kujibishana na mashabiki wa United ambao hawana mpango wa kuisapoti timu yao kutokana na kiwango chake.

“Mfurahie soka,” anasema Mourinho akiwataka mashabiki wa United wapunguze kuzungumzia timu yake mabaya kila muda na kujaribu kuwapa presha wachezaji wao.

Ilifikiriwa kwamba sare dhidi ya Liverpool ingewavutia wachambuzi na kuiona United bora kuliko Manchester City, au kile kipigo walichopata dhidi ya Huddersfield kingeweza kuwaweka katika sinia moja na City ambao hawajafungwa tangu Agosti 21, mwaka huu.

United ambao walicheza na timu ya Chelsea jana ambayo Manchester City waliifunga bao 1-0, mchezo huo utaongeza presha kwa Morinho na timu ya United kama hawatashinda kwa sababu wataongeza pengo dhidi ya vinara wa ligi hiyo.

Katika mchezo dhidi ya Tottenham walimaliza kwa aina yake. Walianza mechi katika kiwango kibovu lakini walimaliza wakiwa mbele kwa ushindi wa bao 1-0 alilofunga Anthoy Martial, akitokea benchi baada ya kupokea pasi iliyopigwa kwa kichwa na Romelu Lukaku.

“Ningependa mashabiki waeleze kwanini hawampi ushirikiano Lukaku kwa sababu anafanya kila awezalo kuisaidia timu, si sawa unapofunga bao au kutofunga bao na mambo yakawa sawa sawa.

“Ukweli kuna vitendo sivielewi kama hawa ni Red Devil? Kuna wakati siwaelewi kwani washambuliaji wanafanya kazi yao vizuri, tulikuwa na wachezaji wawili dhidi ya walinzi watatu kama ambavyo tulifanya tulipokuwa kwenye michuano ya Europa, walifanya kazi ya ukabaji lakini washambuliaji walitupa suluhisho kuepuka presha na kushinda.

“Lakini mashabiki wa klabu walilipia tiketi, hivyo wanaweza kufanya wanavyojisikia, wanaweza kuwazomea wachezaji ambao hawastahili kuzomewa na wanaweza kufanya pia kwa mchezaji ambaye anafanya kazi kama mnyama,” anasema Mourinho.

Mourinho alitaja neno mnyama kama ambavyo mkongwe Sir Alf Ramsey alivyokuwa akimwelezea nyota wa Argentina, lakini ilikuwa zaidi ya Ramsey wakati Mourinho alipokuwa akielezea mchezo dhidi ya Tottenham.

Hata hivyo, hakuna shabiki wa United aliyekuwa akilalamika kwamba  hajafurahia soka la vijana wa Mourinho kwa kumtoa Marcus Rashford na kuingia Lukaku.

Lakini Mourinho aliwataka mashabiki watambue kwamba kiwango cha Lukaku ni bora hasa baada ya kusababisha bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Tottenham.

Katika msimu wa kwanza  ambao  Mourinho aliweza kunyakua mataji mawili, United ilionekana ingeweza  kuonesha ushindani mkubwa katika ligi kwa mara ya kwanza tangu aondoke Sir Alex Ferguson.

Mourinho aliweza kumshawishi Mkurugenzi wa United, Ed Woodward,  apewe majukumu makubwa ndani ya klabu hiyo ikiwa pamoja na kusajili wachezaji ambao atawatumia katika kupata ubingwa kwenye uongozi wake.

“Nafahamu kuna njia tofauti katika kuchambua mambo, kama vile ubora wa baadhi ya klabu, kwa mfano mbinu wanazotumia pamoja na tabia za wachezaji.

“Kwa timu nyingine wakiwa na kiwango kinachofanana inakuwa hali tofauti na sifa nyingi kwao kwa mfano, Tottenham iliwafunga Liverpool mabao 4-1, Real Madrid mabao 3-1 lakini hawakupata bao walipocheza na sisi hivyo wachezaji wangu wanatakiwa kupata heshima yao katika jambo hili,” anasema Mourinho.

Rafiki wa karibu wa Mourinho, Jose Morais, ambaye waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Benfica, Inter, Real Madrid na Chelsea, mwezi uliopita alieleza mtandao wa MEN Sport kwamba, Mreno huyo anaweza kukaa katika klabu misimu mitatu na kuondoka zake.

“Unaweza kuwa na furaha kwa kuwa  unafanya kazi katika mazingira mazuri, unapata matokeo na wakati huo huo familia inakuwa na furaha, kila mmoja yupo vizuri,” anasema Morais.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here