SHARE

LONDON, England 

BEKI wa West Ham, Issa Diop, ni mtu anayetakiwa na kocha wa Tottenham, Jose Mourinho, kwa mujibu wa gazeti la Foot Mercato la Ufaransa. 

Kwa mujibu wa ripoti, Spurs ipo kwenye mazungumzo ya mara kwa mara na wakala wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23. 

Inadaiwa pia Diop amemuulizia mchezaji wa zamani wa Toulouse, Serge Aurier, kuhusu Spurs ikiwa ni mikakati ya kujiunga na klabu hiyo katika siku za usoni.

Hakuna dau lolote lililowekwa mezani lakini inasemekana Diop ameonyesha nia ya kuhama huku West Ham wakifikiria Euro milioni 60 (takribani shilingi bilioni 150).

Foot Mercato inaongeza pia kuwa straika wa Wolves, Raul Jimenez, anawindwa na Mourinho anayepanga kusuka upya kikosi chake hata kama Harry Kane hatakwepo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here